WOLPER AMCHANA 'LIVE' HARMORAPA... ASEMA SOMETIMES 'ANABOA SANA'

JACQUELINE Wolper amefunguka kuwa mwanamuziki chipukizi ambaye hivi sasa amekuwa gumzo mjini, Athuman Omary ‘Harmorapa’ anatia hasira kutokana na kauli zake.

Wolper ambaye ana jina kubwa Bongo Muvi, alisema kinachomuudhi kwa Harmorapa ni kitendo cha mpenzi wake, memba wa Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ kumuongelea vizuri lakini yeye anapohojiwa na vyombo vya habari anaponda.
Harmonize
“Jamani yaani kama huna moyo unaweza ukapasuka kwa hasira maana Harmorapa anaudhi sana, wenzie wakimuongelea vizuri yeye anawaongelea vibaya unafi kiri mtu ataacha kukuchukia? Abadilike,” alisema Wolper bila kutaja lini na kauli zipi Harmonize alimuongelea vizuri Harmorapa.
Hata hivyo, kumbukumbu zinaonesha, hivi karibuni Harmonize aliondoka kwa dharau katika Kituo cha EATV baada ya kusikia Harmorapa alikuwepo eneo katika eneo hilo ambalo naye aliitwa kwa ajili ya mahojiano

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search