BAD NEWS!! Kada mwengine wa CCM Wilayani Kibiti auawa kikatili akiwa nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo !
KIBITI: Mwenyekiti wa CCM tawi la Njia nne liliopo katika kijiji cha Muyuyu, kata ya Mtunda wilayani hapa ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Juma
Njwayo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji.. amemtaja Mwenyekiti huyo aliyefariki dunia kuwa ni
Iddy Seif Kirungi ambapo mwanae nae alijeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi tumboni.
Alimtaja majeruhi kwa jina la Nurdin Iddy Kirungi.
Alisema marehemu alipigwa risasi akiwa
kwake wakati akijaribu kukimbia.
Njwayo alisema kabla ya kuuwawa kwa
Mwenyekiti huyo pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi tumboni
mtoto wa marehemu ambayo ilimjeruhi vibaya na kukimbizwa Hospitali.
Mganga wa zamu katika kituo cha afya
Ikwiriri, Dr Rashid Omar alisema walimpokea Nurdin akiwa na jeraha kubwa
tumboni mwake ambalo halikutokeza upande wa pili.
Alisema majeruhi huyo walimpatia rufaa
kwenda Hospital ya Mchukwi kutokana na kuwa anavuja damu nyingi sana...
...endelea kubofya: www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com
kwa habari mpya kila tunavyozipokea.
No comments:
Post a Comment