Dunia yaadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari!
MEI 3 ya kila mwaka imetengwa maalumu na Umoja wa Mataifa (UN) kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Siku hii iliidhinishwa kwa mara ya kwanza na umoja huo mwaka 1993 kutokana na mabadiliko makubwa ya kisiasa na uchumi duniani.
![]() |
| Waziri Mwakyembe |
Lengo la siku hii ni
kuangalia changamoto zinazokabili waandishi na mazingira wanayofanya kazi kama
yanaridhisha au la,na kutambua pia mchango wa waandishi waliopigania taalamu ya
uandishi wa habari hadi tone la mwisho la maisha yao.
Kwa lugha nyingine ni
siku muhimu kwa waandishi wa habari kutathmini na kupitia changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta hiyo duniani. Hata hivyo, wakati siku hii ikidhimishwa
jambo la kusikitisha ni kuwa vyombo vya habari vinafanya kazi katika kipindi
kigumu hususan Afrika.
Sababu kubwa ni kwamba
viongozi wengi wanaviona vyombo hivyo kama adui wao wakati kwa vile tu vinasema
mambo ya ukweli. Ndiyo maana waandishi wanakamatwa, kushtakiwa na wakati
mwingine maisha yao kuwa hatarini kutokana na kazi wanayofanya.
Ripoti ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani ya mwaka huu (2017) imeeleza mengi kuhusu hali halisi
ya vyombo hivyo ilivyo duniani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo Namibia, Ghana na
Cape Verde ndiyo zinazotoa uhuru mkubwa kwa vyombo vya habari kwa upande wa
Afrika. Hii maana yake kinachoendelea katika mataifa mengine ya Afrika ni
ukandamizaji wa uhuru wa habari. Hii si habari njema hata kidogo.
Matokeo yake ni kwamba
viongozi hawataki kuambiwa ukweli hata kama wanaongoza nje ya misingi ya
utawala bora na sheria.
·
Nchi ambazo hazizingatii misingi hiyo kusema
kweli maendeleo huwa duni na ujenzi wa utawala wa kidemokrasia hukosa mwenyewe.
·
Amani ndani ya nchi na mtu mmoja mmoja hufifia
na watu kuishi kwa hofu kwa sababu tu ya kuwa na viongozi ambao si rafiki wa
vyombo hivyo.
·
Ni katika mazingira hayo vyombo vya habari
vinafanya kazi kwa kuchechemea na wakati mwingine vingine kukuta vikifungwa.
·
Si hivyo tu bali ni Afrika hii viongozi hutumia
nguvu kubwa kutengeneza sheria kali ili vishindwe kufanyakazi kwa uhuru unaotakiwa.
·
Viongozi wanasahau kuwa bila uhuru wa vyombo vya
habari hakuna maendeleo endelevu kwani mambo mengi hufanyika gizani.
·
Nchi zinazobana uhuru wa waandishi huishia
kutumia nguvu nyingi katika mambo yasiyostahili na uonevu hutawala.
Ni kwa nini tunashindwa
kujifunza kutoka nchi nyingine namna zinavyotoa uhuru mpana kwa vyombo vya
habari na hakuna kinachoharibika?
Ripoti hiyo inasema
Norway, Sweden, Finland zimeendelea kufanya vizuri katika kutoa uhuru wa vyombo
hivyo pamoja na waandishi.
Ni lazima tukumbuke
kuwa kukandamiza vyombo vya habari ni sawa na kuruhusu shetani kutamba altareni
jambo ambalo si sahihi hata kidogo.




No comments:
Post a Comment