Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania latoa kauli nzito dhidi ya hali ya vurugu, mauaji na uvunjifu wa amani unolikumba Taifa hivi sasa....#share
BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania limelaani matendo ya vurugu, mauaji, na uvunjifu wa amani yanyoendelea nchini huku likibainisha kuwa hali hiyo inalifedhehesha Taifa.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Tundu Lissu kupigwa risasi mkoani Dodoma na watu wasiojulikana lakini pia wiki kadhaa baada ya ofisi za IMMMA Advocates kulipuliwa na mabomu.
Taarifa iliyotolewa kwa umma mapema na Baraza hilo imebainisha kuwa kwa sasa nchini kumeshuhudiwa matendo ya mauaji ya watu wasio na hatia maeneo kama ya Mkuranga, Rufiji na Kibiti, utekwaji wa watu na kuteswa, utekaji wa watoto, Ulipuaji wa ofisi na shambulio dhidi ya Mbunge Lissu.
"Tunapenda kutamka wazi na kwa nguvu zetu zote kuwa vurugu na mashambuya aina yoyote ile yanalifedhehesha Taifa. Matendo haya ni Dhambi, uhalifu na si utamaduni wetu. Tunaomba yakomeshwe mara moaja,@

No comments:
Post a Comment