Forbes Yatangaza wanamuziki ‘vibopa 25’ Duniani,.. JAY Z, P. Diddy wachuana vikali !
Utajiri wa mwanamuziki Jay Z ulipanda kwa asilimia 30
mwaka jana na kufikisha utajiri wake hadi $810m (£626m), kwa mujibu wa jarida
la Forbes.
Lakini kuimarika kwa utajiri wake hakukutosha kumuondoa
Sean "Diddy" Combs kutoka kwenye kilele cha wanamuziki matajiri zaidi
wa Hip Hop kwa mujibu wa jarida hilo.
Diddy
anaongoza akiwa na utajiri wa jumla ya $820m (£633m).
Forbes
walisema utajiri wake ulioimarishwa na mikataba ya kibiashara ambayo alitia
saini na Diageo kwa ajili ya Ciroc vodka na mavazi yake ya Sean John.
Lakini
rapa na produsa Jay Z alipanda hadi nafasi ya pili sana kutokana na uwekezaji
wake wa $200m (£155m) katika kampuni ya kuuza muziki mtandaoni ya Tidal.
Pia,
ana mvinyo kwa jina Armand de Brignac, na anamiliki pia Roc Nation.
Mwaka
uliopita, utajiri wa Diddy ulikuwa $750m (£579m) na wa Jay Z $610m (£471m).
Forbes waliandaa orodha yao wakizingatia mapato ya miaka ya nyuma pamoja na stakabadhi za kifedha, thamani ya mali inayomilikiwa na wanamuziki hao na pia kwa kuzungumza na wachanganuzi, mawakili, mameneja na wataalamu wengine katika tasnia ya muziki.
Rapa wa zamani wa NWA Dr Dre kwa sasa ana utajiri wa $740m (£571m) baada ya kuuza Beats kwa Apple mwaka 2014 kwa $3bn (£2.3bn), lakini amepitwa na Jay Z kwa mara ya kwanza.
Baada ya kuuza Beats, alinunua jumba kubwa la kifahari Los Angeles la ukubwa wa futi 14,000 mraba kwa $40m (£31m).
Rapa ambaye pia ni mmiliki mwenza wa Cash Money Records Bryan "Birdman" Williams ana utajiri wa $110m (£85m).
No comments:
Post a Comment