Picha 4: Miaka 20 ya Kifo cha Diana, Princess of Wales Jinamizi Kuu limemshukia kaka yake Earl Spencer !!

Wakati Waingereza na Dunia ikikaribia kuadhimisha miaka 20 ya Kifo Cha Princess Diana, Mama wa Mrithi wa Mfalme Prince William wa Uingereza, Jinamizi limemkumba kaka mkubwa wa Diana, ambae amedai kuna kampeni mbaya ya Kumdhalilisha.

Kaka huyo Earl Spencer amedai amedaka siri ya kipindi kinachopangwa kurushwa na Television ya Chanel 5, ikielezea tabia aliyoonyesha siku ya Mazishi ya Diana ambapo alisusa kusimama mbele ya Jeneza la dada yake pamoja na Wana Ukoo wa Kifalme kama ishara ya kumuenzi, na ameapa kwenda Mahakami kutaka kipindi hicho kisimamishwe na kuondolewa baadhi ya vipengele kadhaa vinavyomkashifu.

Diana, aliefariki akiwa katika harakati za kukwepa 'mapaparazi' akiwa na Mpenzi wake Dodd Alfayeed Jijini Paris Nchini Ufaransa, mbali na sifa kuu ya uzuri na ulimbwende uliopindukia, alijijengea umaarufu kwa tabia yake ya kuogopa Kamera hata kwenye matukio ya kawaida, huku akitumia pochi yake ndogo ya mkononi kama sehemu ya kujifichia...(nimeambatanisha picha zake angalia anavyojitorosha ili wapiga picha wasimuone)

Spencer alivyoulizwa kwa nini hakutaka Ukoo wa Kifalme usogelee Jeneza na Dada yake alijitetea kwamba alifanya hivyo kumlinda mpwa wake Harry ambaye kwa umri wake wa miaka 12 hakustahili kuekwa katika mstari wa mbele kwenye shughuli za uagwaji wa mwili wa mama yake... "Hali ya mambo nchini hapa huendeshwa kwa matakwa ya watu fulani fulani,.. na ilibidi nikubaliane na uhalisia.. sikuwa na namna nyengine..." alimalizia Spencer.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search