Ramadhan Offer: From zantel...

Wateja wa mtandao wa simu Zantel sasa kufurahia mawasiliano na ndugu jamaa na marafiki waliopo  mashariki ya kati kwa bei nafuu kwa kutumia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni.
………………………………………………..
Kampuni ya simu ya Zantel inaendelea kutimiza ahadi yake ya kuongeza thamani katika maisha ya wateja wao na sasa kutangaza ofa maalum inayowalenga waumini wa dini ya Kiislamu nchini ili kuadhimisha mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani duniani kote.
Akitangaza habari hii makao makuu ya kampuni ya Zantel yaliyopo Msasani jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Zantel Bw. Benoit Janin amesema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki na ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao”.
Aliongeza kwa kusema mtandao wa Zantel utaendelea kutoa huduma kwa mamilioni ya Watanzania kuwasaidia kutimiza malengo na ndoto zao kupitia vipengele mbali mbali vya huduma za kampuni hiyo ikiwa ni pamoja bidhaa na huduma za  upigaji simu, vifurushi vya internet na mtandao. Alisema kampuni itahakikisha vyote hivi kwa kutoa huduma na bidhaa bora za upigaji simu na vifurushi vya intaneti huku tukihakikisha tunawekeza faida endelevu. Kwa mwaka 2016 kulikua na matatizo mbali mbali ila kwa sasa mkakati wetu ni kuhakikisha tunatoa vipao mbele kwa vitu vyenye umuhimu mkubwa kwa wateja ikiwemo kuwa mtandao bora unaotoa intaneti ya kasi zaidi wa 4G, kupenya na  kuwafikia watumiaji wengi zaidi,na kujiandaa kwa siku zijazo kuwa kampuni ya bidhaa inayopendwa zaidi.
“Tunahitaji kuwa tayari kwa siku zijazo kwa njia mbali mbali za kuongeza mapato pamoja na huduma zinazoongeza thamani ya mtandao wa zantel ikiwemo uboreshaji wa vifurushi vya intaneti, tayari tunaona mabadiliko makubwa katika mtandao wetu” aliongezea kwa kusema “Kutakua na bidhaa mbali mbali tutakazozitoa kipindi hiki zitakazofurahiwa na wateja wetu kukiwa na mpangilio wa ofa zilizoanza tarehe 24/05/2017” Aliongezea.
Akielezea zaidi kuhusu ofa hii, Mkurugenzi wa masoko wa Zantel Bw. Gasper Mbowa amesema”Ofa hii ya Ramadhani imelenga kuwazawadia wateja wetu wa malipo ya kabla watakaojiunga na vifurushi vyetu kwa kiasi chochote au kwa kuongeza muda wa maongezi kwenye  kipindi cha mfungo wa Ramadhani. Mteja yoyote atakayeongeza mda wa maongezi atapata asilimia 50 ya muda wa maongezi moja kwa moja utakaomuwezesha kupiga simu Zantel kwenda Zantel, ofa hii itakua inatumika kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi. Vivyo hivyo wateja wataweza kutumia huduma zetu zilizozinduliwa hivi karibuni kama ‘Zantel madrassa itakayowawezesha kujifunza dini ya kiislamu kwa kupokea mafunzo ya Quran, hadith, dua, habari za BAKWATA na huduma nyingine nyingi kwa kupitia simu zao za mkononi kupitia ujumbe mfupi wa maneno au kwa kupiga simu.
Mbowa aliongezea kuwa wateja wa Zantel wanaweza kuwapigia simu ndugu, jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu zaidi kupitia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni. “Kwa shilingi za kitanzania 2,000 wateja watapata dakika 4 za kupiga simu  Qatar, Oman, UAE, Lebanon, Pakistan, Yemen & Saudi Arabia, na kwa shilingi 5,000 watapata dakika 7 kupiga simu kwenda kwenye  nchi tajwa, na fedha hizo zitakatwa moja kwa moja kwenye akaunti zao”
Vifurushi vyote hivi vitapatikana kwa kujiunga kwa kupiga *149*15# na kwa vifurushi vya ‘Bonga Mpakabasi’, ‘Zantel Madrassa’ wateja wataweza kujiunga kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kutumia neno SUB na kutuma kwenda namba 15586 au kwa kupiga namba 15586

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search