TAKUKURU wataja vinara wa Rushwa Temeke

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ Mkoa wa Temeke imezitaja taasisi ambazo zinaongoza kwa kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa ndani ya tisa iliyopita ikiongozwa na Halmashauri ya Temeke.
Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Temeke Pilly Mwakasege amezitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Manispaa ya Temeke, Mahakama, sekta binafsi, Polisi, Ardhi, Afya na Idara nyingine. Mpaka sasa TAKUKURU imefungua mashauri mapya matatu Mahakamani huku mashauri manne yakiwa yanaendelea kusikilizwa Mahakamani katika hatua mbalimbali huku ikiokoa zaidi ya Tsh. 99m ikiwemo mishahara hewa na kujilipa posho isiyo halali ndani ya miezi hiyo tisa. 
Bofya hapa kumsikiliza kamanda mkuu wa TAKUKURU kanda ya Temeke:-blessnewstz

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search