Mtaa wa Victor Wanyama wazua tafrani Ubungo,.. #Serikali yang'oa Bango !!!

Leo hii kumekuwepo na hisia anuwai miongoni mwa wakazi wa Ubungo na watumiaji wa mitandao ya kijamii juu ya uamuzi wa ofisi ya Meya Chadema kuamua kuutunuku mtaa mmojawapo jina kwa heshima ya mchezaji hodari wa mpira wa miguu Nchini Mkenya Victor Wanyama.
Matukio imefanikiwa kunasa picha ya anaesemeka mtu aking'oa bango maalumu linaloutambulisha mtaa 'Road Signage' ikisemekana limeg'olewa kwa amri ya Serikali !

Katka tukio jengine mtu aliejitambulisha Kwa jina la JS kutoka kambi ya Upinzani alihamishia hasira zake zote kwa uongozi wa kitaifa uliopita madarakani bila kutaja jina anamzungumzia nani ingawa waswahili husema mwenye macho.....!
Nae mtumiaji Mwengine maarufu mtandaoni alitusogeze ufafanuzi kutoka uongozi wa Wilaya Na Manispaa ikikosoa vikali kitendo Cha kutaja majina mitaa bila kufuata taratibu husika..

"UFAFANUZI KUHUSU MAKOSA YALIYOFANYWA NA VIONGOZI WA KATA YA UBUNGO KUMPA MTAA VICTOR WANYAMA

Majina ya mitaa hupendekezwa na kamati za mitaa husika kisha hupelekwa kwenye vikao vya WDC vya kata halafu maamuzi ya WDC hupelekwa kwa Mkurugenzi kwa ajili ya kuingizwa kwenye kikao Cha kamati ya Fedha na uongozi, Baraza la Madiwani, halafu DCC,  RCC na Kisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na baadaye kwa Mchapaji mkuu wa serikali na mwisho hutokea kwenye Tangazo la serikali GN. 

Na hapo ndipo mtaa hujulikana huo ni mtaa fulani. Taratibu za kubadili pia lazima zifuate hatua hizo muhimu.

KILICHOFANYIKA NI KINYUME NA UTARATIBU WA KISHERIA"

Imetolewa Na; 
Kitengo Cha Habari na Uhusiano 
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search