Professor PLO Lumumba asema 'Magufuli saafiii' #share asema ndani ya miaka 10 Tanzania itapaa kiuchumi!!!

Dar Es Salaam. Profesa Patrick Lumumba ameusifia uamzi wa Rais John Magufuli  katika vita yake ya kiuchumi na kusema kuwa endapo hali itaendelea kuwa hivi kwa miaka 10 ijayo Tanzania itakuwa ni nchi kubwa sana kiuchumi barani Afrika.


Profesa Lumumba amesema hayo leo katika Kongamano la kigoda cha Mwalimu ambapo alialikwa kwaajili ya kuzungumzia kipengele cha Siasa safi ndani ya Afrika ambayo ilikuwa ni mada ndogo kutoka mada kuu ya mwaka huu isemayo 'Nafasi ya wanasiasa katika kuanguka na kuinuka kwa maendeleo ya Afrika..'

"Japo mimi sio mwana CCM lakini namsifu Magufuli amonyesha kulinda Rasilimali za nchi yake Mungu ambariki, Amewafanya wanaoitwa Acacia wakatubu na kukubali kosa naye akawasamehe kwa kuwaambia kuwa shariti ni kulipa," anasema.

Anaongeza kuwa hata uamzi wa kuwalinda marais wastaafu katika sakata hilo ni zuri kwakuwa mtu ukitaka kuendelea ni lazima usamehe mhimu ni kukumbuka na kumbukumbu sio zote bali baadhi yake.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search