Ripoti ya Makinikia ya Prof. Osoro yazua mambo... yamkwaa Ngeleja Bungeni... #share.. yeye asema...

Baada  ya kutajwa miongoni mwa wanaotakiwa kuchunguzwa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema maisha yanapaswa kuendelea.

Mhe. Ngeleja katika moja ya matukio akiwa kikazi zaidi 
Ngeleja amesema hayo leo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali baada ya Mbunge wa Mbunge wa Mbozi kuomba taarifa ya kutajwa kwa Mbunge hiyo wa Sengerema kutajwa kuhusika kulitia taifa hasara kutokana na mapato ya madini.

Ingawa Mwenyekiti wa Kikao, Mussa Azzan Zungu aliikataa taarifa hiyo, Ngeleja alisema: "Kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia, maisha yanaendelea."

Baada ya maneno hayo machache aliendelea kutoa mchango wake. Hii ni Mara ya kwanza kwa mbunge kuzungumzia, japo kwa kifupi, kuhusika kwake kwenye udanganyifu uliobainika kufanywa na kampuni za madini nchini.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search