SportPesa SuperCup (3 - 0) - Gor Mahia wababe kwa ndugu zao AFC Leopards

Baada ya mbio ndefu za michuano ya SportPesa Super Cup hatimaye Jumapili hii Klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya wamechukua kombe hilo kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya mahasimu wao, AFC Leopards.
Gor Mahia wamepata goli lao kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Otieno Philemoni kunako dakika ya 18 kipindi cha pili. Timu hiyo iliongeza kasi zaidi na kujipatia magoli mengine wawili na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa kuwafunga Leopard goli 3 kwa nunge.
Gor Mahia kwenye safari yake mpaka kufika fainali ya SportPesa Super Cup imezitoa klabu za Jang’ombe Boys kutoka Zanzibar na Nakuru All Stars .
Kwa ushindi huo klabu ya Gor Mahia imeibuka na kitita cha Dola elfu 30,000 za kimarekani na imepata nafasi ya  kuchuana na Klabu ya Everton kutoka England Tarehe 13 July mwaka huu.
Michuano ya SportPesa Super Cup imeandaliwa na Kampuni ya kubashiri ya SportPesa ambao ni wadhamini wa Klabu za Simba SC, Yanga SC pamoja na Singida United zote kutoka Tanzania na jumla ya timu 8 zilishiriki michuano hiyo ambapo timu zote nne kutoka Tanzania zilitolewa. Bongo5

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search