Video: Kamishna aelezea hali ya kutisha maafisa wa kitengo walivyonasa magunia 168 ya 'Bhange' #share

Maafisa wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawaya kulevya mkoani Arusha wamekamata magunia 168 ya bangi kijiji cha Losinoni wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha

Kamishna wa intellijensia ya mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya Fredy Kibuta amewaonya wauzaji wa dawa za kulevya kusoma alama za nyakati na amewafananisha na 'wauaji'.

Tume ya kupambana na madawa ya kulevya imesema inaendesha operesheni endelevu ya kudhibiti na kupambana na mihadarati ambayo haitamuacha mtu, na kuwataka wananchi kubuni miradi mbali mbali ya kujipatia riziki na kuachana na biashara hiyo ambayo ni hatarishi kwa kizazi cha watanzania.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search