Video: Kauli ya Bulaya na Halima Mdee baada ya Spika kubariki 'kivungo cha mwaka mmoja' nje ya Bunge !!

"Kimya kingi kina mshindo mkuu.." wahenga walisema... bila shaka ungeshangazwa na ukimya wa Wabunge machachari Halima Mdee na Ester Bulaya baada ya Bunge chini ya Uongozi wa Mhe. Spika Ndugai kubariki adhabu ya 'kifungo cha mwaka mmoja nje ya Bunge' kwa wabunge hao kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Capt. George Mkuchika kuwatia hatiani kwa kosa la vitendo vya mara kwa mara vya kulidharau Bunge.

Hatimae, mara baada ya Msiba wa Mzee Ndesamburo jana.. Wabunge hawo vijana wakisapotiwa na Mhe. Tundu Lissu ambae ndie Mwanasheria Mkuu wa Chadema na mnadhimu mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Tundu Lissu,  wameibuka na kuponda vikali adhabu hiyo na kuapa 'kuichallenge' mahakamani. 

Msomaji wa Matukio kwa hisani kubwa ya global na mcl digital, tumekuwekea video hizi mbili uweze kupima uzito wa misimamo yao.. Jee kwa mtazamo wako.. wana haki ya kwenda mahakamani kwa waliyoyatenda au wameonewa ? 

Video: Msimamo wa Mhe. Halima na Bulaya 
Msikilize Tundu Lissu akitoa Msimamo !
 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search