BREAKING NEWS!! Ajira Feki,.. JWTZ yashusha Rungu kwa Vishoka.. #SHARE.. "wasema OLE wao tukiwakamata.."

Jeshi la wananchi (JWTZ) limetoa tahadhari kwa umma juu ya uwezo wa matapeli wanaowalaghai wananchi kwamba watawapatia ajira katika jeshi hilo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Meja Jenerali Harrison Masebo; Katika moja ya Matukio na Waandishi wa Habari

Baadhi ya Askari wa JWTZ wakiwa kwenye mazoezi maalum !
Akitoa tahadhari hiyo, Mkuu wa Utumishi wa JWTZ, Meja Jenerali Harrison Masebo amesema wamepokea malalamiko mengi ya wananchi kuhusu utapeli huo na kusisitiza kwamba jeshi lina utaratibu wake wa kuajiri na siyo kuwatumia watu wengine kufanya kazi hiyo.

Masebo amesema wanawatafuta watu hao kwa sababu wanalichafua jeshi kwa kujiita maofisa wa JWTZ na kujenga dhana kwa wananchi kwamba wametapeliwa na jeshi.

"Tunaomba ushirikiano wa wananchi ili tuweze kuwakamata watu hao. Mtu akikwambia anataka kukupa kazi JKT au JWTZ wewe msikilize lakini tuletee taarifa kabla hukampa chochote, sisi tutamkamata,", amesema Masebo.

Mkuu huyo wa utumishi jeshini amesema ajira zote zinazotelewa na JKT lazima zitangazwe kwenye vyombo vya habari na mchakato wake uko wazi kwa sababu wanaochukuliwa wanachaguliwa kuanzia ngazi ya vijiji, vitongozi, mitaa mpaka wilayani. Amewataka wananchi wasiwape chochote matapeli hao badala yake watoe taarifa jeshini.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search