Exclusive ya Kibatala kumuhusu Tundu Lissu!! 'Tuna Imani na Busara za Jeshi la Polisi..'

WAKILI Peter Kibatala anayemtetea Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amesema endapo hatafikishwa kesho mahakamani wataendelea kushinikiza ombi hilo.


Lissu alikamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  Julai 20 mwaka huu kwa tuhuma za uchochezi, na hadi sasa anaendelea kushikiliwa bila kufikishwa mahakamani kwani kwa mujibu wa sheria angetakiwa afikishwe ndani ya masaa 24.

Akizungumza na Matukio360 leo Kibatala alisema kuwa Rais huyo wa TLS anaendelea vizuri.

Ameeleza kuwa Imani yao ni kwamba  jeshi hilo litatumia busara na kumfikisha mahakamani kama walivyopeleka ombi hilo Mahakama kuu mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Kwanza amekwisha kaa kituoni zaidi ya muda wa kiseria, tunaimani watatumia busara na kumpeleka mahakamani,” alisema Kibatala.

Aidha amesema kuwa wanaendelea kusisitiza apelekwa mahakamani ili kama kunawatu ambao wanamtuhumu kufanya kosa la uchochezi mahakama iweze kuthibitisha shutuma hizo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Mawakili wanaomtetea Lissu wakiongozwa Fatma Karume walipeleka ombi Mahakama kuu kushinikiza afikishwa Mahakamani ili aweze kusomewa mashataka au aachiliwe huru na jeshi la polisi.

Alisema waliamua hivyo kutokana na kwamba alikuwa amekwisha hojiwa lakini Polisi wakadai kuwa bado upelelezi unaendelea huku ikifahamika kwamba kwa mujibu wa sheria ili mtu akamatwe upelelezi unakuwa umekwisha fanyika.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search