Kanisa la Kakobe linahifadhi fedha kwenye ndoo, jaba amuomba radhi Magufuli....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Salha Mohamed, Dar es
Salaam
MAMLAKA ya Mapato Tanzania
(TRA) imesema kanisa la Full Gospel
Bible Fellowship,linaloongozwa na Zacharia
Kakobe linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na majaba kinyume na
taratibu za utunzaji wa fedha.
Pia imesema Kakobe aliandika
barua kwa rais John Magufuli kuomba radhi kufuatia kauli yake ya kebehi na matamshi ya dharau kwamba anafedha nyingi
kuliko serikali.
Kamishna mkuu wa TRA, Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
Kamishna mkuu wa TRA,
Charles Kichere amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kwamba askofu Kakobe
hana fedha wala akaunti nchini ila ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti za
kanisa (Signatories) zilizopo kwenye benki ya NBC zenye kiasi cha sh bilioni 8.
Amesema kanisa hilo linaweka na kutoa fedha nyingi kutoka benki bila kushirikisha
vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha na wahusika.
Kichere amesema kanisa hilo halitengenezi
hesabu za mapato na matumizi ya fedha kinyume
na katiba ya kanisa na sheria za
usimamizi wa fedha na kusababisha matumizi mabaya ya fedha za waumini kama
safari za nje zinazoaminiwa na kanisa huku wanaosafiri ni Kakobe na familia
yake.
"Vile vile fedha za
kanisa zinatumika kujenga nyumba ya mke
wa askofu kwa jina lake wala si jina la kanisa jambo ambalo ni kinyume na
taratibu za kanisa," amesema Kichere na kuongeza
"Wakati uchunguzi ukiendendelea Januari 24,2018 Askofu Kakobe
aliandika barua kwa rais John Magufuli
kuomba radhi kutokana na kauli yake ya kebehi pamoja na matamshi ya dharau
kwamba anafedha nyingi kuliko serikali.’’
Kamishna huyo amesema uchunguzi umebaini kiasi cha sh bilioni
8 za kanisa hilo zimetokana na sadaka, zaka na changizo ambazo
zinatolewa na waumini wa kanisa na kwa
mujibu wa sheria hazitozwi kodi.
Amesema kanisa lilikwepa kulipa kodi ya sh milioni 20 zilizotokana na uwekezaji katika makampuni ya
kukuza mitaji.
Ameongeza kuwa, Kampuni
inayomilikiwa na watoto wa Askofu Kakobe ilikwepa kulipa kodi sh milioni 37.
"Kutokana na uchunguzi
fedha zote walizokwepa kodi sh milioni 58 pamoja na faini
zimelipwa,"amesema.
Kichere ametoa wito kwa
taasisi za dini zinazojihusisha na shughuli za kiuchumi kulipa kodi stahiki kwa
wakati kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kodi.
"Mamlaka ya mapato
Tanzania inazitaka taasisi zote za kidini kufuata katiba zao ikiwa ni pamoja na
kutengeneza hesabu za mapato na matumizi, "amesema Kichere.




No comments:
Post a Comment