Utoro Temeke: Kamanda Gilles awahesabia siku waalimu... ataka wampe ripoti kamili.. #share
KAMANDA wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke,Gilles Muroto amewapa siku chache waalimu wa Mkoa huo wa kipolisi kurejesha marejesho juu ya ufatiliaji wa wanafunzi watoro shuleni.
Akizungumza leo katika Dae es Salaam katika Mkutano uliowakutanisha waalimu wa Mkoa wa Kipolisi Temeke amesema kila mwalimu anawajibu wa kujua maendeleo ya wanafunzi wake pindi wanapokuwa na maadhurio mazuri shuleni.
"Wajibu wa wazazi,walezi na waalimu kujua kwa kutambua mwenendo wa mwanafunzi kwanini maudhurio yake mabaya au kushuka kiwango chake cha ufaulu,"alisema Muroto.
Amesema oparesheni yetu ya kukamata wazazi itasaidia kupungunza utoro wa wanafunzi kwa sababu wazazi wakiea wakali wanafunzi watakuwa na maudhurio mazuri na watajiepusha kujiingiza katika makundi ya uhalifu.
Aidha amewata waalimu kufatilia mwenendo wa wanafunzi watoro ili kuweza kuwakamata wao pamoja na wazazi wao.
Amesema wanafunzi kumi na 16 waliokuwa eanashikiliwa na Jeshi hilo wamekwisha achiwa na kurudi shuleni huku wazazi 10 wao kupandishwa mahakama kwa kukiuka sheria ya mtoto.
Dalila Sharif.
No comments:
Post a Comment