bAD nEWS: Watu 6 wafariki na wengine 42 kujeruhiwa kwa ajali ya lori Mkoani Singida kijiji cha Kijota..#share
WATU sita
wamefariki dunia huku wengine 42 wakijeruhiwa baada ya lori lenye namba za
usajili T.806 AEL aina ya Scania mali ya Abdalla Mussa (39) mfanyabiashara
mkazi wa Mwenge mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha
Kijota, Singida.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Singida, ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo imetokea
Agosti 27 mwaka huu saa 1.30 usiku katika kijiji cha Kijota
wakati likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini,
likielekea Singida mjini.
ACP Magiligimba
ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka
(32) ambaye hakuwa makini wakati akiendesha lori hilo lililosheheni abira na
mizingo.
Amewataja
waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Haji Jumanne (35), Mikidadi Mohammed (40)
wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama na Musa Salimu (30) mkazi wa kijiji cha
Mwakiti.
Wengine ni
Allen Mwangu (38) mkazi wa Wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano (40) mkazi wa
Kijiji cha Mrama na Sharifa Omari (19) mkazi wa Kijiji cha Ilongero.
Kamanda
Magiligimba ameongeza kuwa majeruhi 20
wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, kumi wamelazwa hospitali ya
misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa katika hospitali
ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.
Ameeleza
kuwa baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu na kurejea makwao huku wengine
waliolazwa wamevunjika mikono, miguu na sehemu mbalimbali ya miili yao.
“Hawa
wenye hali mbaya ni Fadhili Jumanne (33) mkazi wa Kibaoni mjini Singida,
Mikidadi Hamisi, Jafari Hamisi na Idrisa Ibrahimu, wote wamevunjika miguu.
Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali misheni Mtinko,” alisema.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment