nEWS: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka wawekezaji wanaotaka kuwekeza nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu...#share


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watu wote wenye nia ya kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu. 



Alitoa kauli hiyo jana alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais (Uendelezaji Bishara) wa Kampuni ya PIRIOU, Michel Perrin. 

Waziri Mkuu alikutana na Perrin jijini Paris nchini Ufaransa kupitia Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Kampuni ya PIRIOU inataka kuja nchini kuwekeza katika utengenezaji na ukarabati wa meli. 

Akizungumza na muwekezaji huyo Waziri Mkuu alimshukuru kwa nia yake ya kutaka kuwekeza nchini, ambapo alimtaka afuate sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji nchini. 

“Tanzania ni sehemu nzuri ya uwekezaji kwa sababu kuna fursa nyingi. Pia ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo nakukaribisha sana,”alisema. 

Kwa upande wake, Perrin alisema ameamua kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi salama na kwamba anauhakika wa kupata soko ndani ya nchi pamoja na mataifa jiraji. 

Alisema anaamini uwekezaji wake nchini Tanzania utakuwa na tija, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali na pia atahakikisha anafuata sheria zote za nchi.

Perrin alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Balozi Samuel Shelukindo kutokana na ushirikiano anaompa kuhusu masuala ya uwekezaji nchini.

Naye Balozi Shelukindo alisema ataendelea kutafuta wafanyabiashara mbalimbali na kuwashawishi waje kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search