bREAKING nEWS: Mbunge Rwakatare afutiwa shitaka la Ugaidi.. DPP asema hana nia ya kuendelea nalo.. #share

Kesi ya shambulizi la kudhuru  iliyochukua muda mrefu kati ya Mwandishi wa Habari maarufu Bw. Dennis Msaky dhidi ya aliekuwa afisa mwandamizi wa kitengo cha propaganda ndani ya CCM Bw. Rwakatare, imefikia tamani baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuondoa  maombi yake kuhusiana na shtaka la ugaidi dhidi ya Bw. Rwakatare ambae kwa sasa ni Mbunge wa Bukoba mjini.



Maombi hayo ya DPP yaliyokuwa yamefunguliwa Mahakama ya Rufani kuomba mapitio ya  maamuzi ya Mahakama Kuu kumfutia shitaka la Ugaidi Bw. Rwakatare, yalitarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufani Mussa Kipenka, lakini DPP akaamua kuyaondoa kabla ya usikilizwaji.

Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, ameieleza mahakama kuwa DPP hana nia ya kuendelea na maombi hayo.

Kutokana na nia hiyo ya DPP, wakili wa mjibu maombi, Richard Rweyongeza amesema kuwa hana pingamizi dhidi ya nia ya DPP kuyaondoa maombi hayo, na Jaji Kipenka akatoa amri ya kuyaondoa mahakamani maombi hayo.

Kwa uamuzi huu sasa Lwakatare anabaki na shtaka la kula njama ili kutenda kosa, katika kesi ya msingi inayosikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Awali Lwakatare na mwenzake walikuwa Ludovick Rwezaura, walikuwa wakikabiliwa na jumla ya mashtaka manne likiwemo la kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi kwa lengo la kumdhuru kwa sumu aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.

Mashtaka mengine yalikuwa ni ya ugaidi, wakidaiwa kuandaa mikutano ya kupanga makosa ya kigaidi na kufadhiri vitendo vya kigaidi.

Hata hivyo Lwakatare kupitia kwa mawakili wake walifungua maombi Mahakama Kuu wakipinga.mashtaka hayo yaliyokuwa yakiangua katika Sheria ya Ugaidi.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Lawrence Kaduri ilikubaliana nayo na akamfutia Lwakatare mashtaka hayo ya ugaidi na hivyo kubakiwa na shtaka moja tu la kula njama ambalo haliangukii katika sheria hiyo ya ugaidi.

DPP hakukubaliana na uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ndipo akafungua maombi ya kibali kufungua maombi nje ya muda, ili kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kumfutia mashtaka hayo ya ugaidi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search