GUMZO: Hali ya Afya ya Mbunge Esther Bulaya yazorota akiwa rumande,.. achomolewa na kulazwa Hospitalini.. #share
Baada ya kuingia 'matatani' na kutiwa rumande, Mbunge wa Bunda mjini Esther Bulaya amelazimika kutolewa kwa muda na kukimbizwa na kulazwa katika Hospital moja ya Mjini wa Tarime kutokana hali yake ya afya kubadilika akiwa katika kituo kikuu cha polisi alipokuwa amezuiliwa.
Mwenyekiti cha Chadema Wilaya ya Tarime Lucas Ngoto amesema Bulaya amelazwa kutokana na matatizo ya Kifua kubana.
"Mheshimiwa Bulaya anamatatizo ya kifua kubana hivyo hali yake ilibadilika kutokana na hali ya kule rumande na Saa moja usiku huu akawa amepelekwa hospitalini na kulazwa wodi namba nane," amesema Ngoto.
Bulaya alikamatwa Jana jumamosi saa tisa alasiri na jeshi la polisi Wilayani Tarime mkoani Mara na kuhojiwa kwa zaidi ya saa matatu kabla ya kupeleka Rumande ambapo hali yake ya afya imeanza kuzorota.



No comments:
Post a Comment