Polisi wasema upelelezi kesi ya Lowasa haujakamilika # Atakiwa kurudi Julai 20... #share
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA, Edward Lowassa ametakiwa kuripoti tena Ofisi ya Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Alhamisi ya juma lijalo kutokana na
upelelezi kutokamilika.
Lowassa
alifika ofisi ya DCI kama alivyotakiwa kuripoti na baada ya kukaa nusu saa
ndani alitoka na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zake kutokana na upelelezi wa
kosa linalomkabili la kutoa kauli za kichochezi kutokamilika.
Mwanasheria wa Lowassa, Peter
Kibatala amewaambia wanahabari kuwa wamearifiwa na DCI kwamba upelelezi wa
tuhuma hizo bado haujakamilika.
"Lowassa kama alivyoambiwa na
uongozi wa jeshi la polisi ofisi ya DCI maelekezo ni kwamba turudi au arudi
tena Alhamisi ya Julai 20 mwaka huu saa 3:00 asubuhi. Tutarudi tupate maelekezo
zaidi', amesema Kibatala.
Lowassa aliingia matatani baada ya
kuhoji hatua ya serikali kuendelea kuwashikilia masheikh wa kundi la uamsho
bila ya kuwafikisha mahakamani kwa zaidi ya miaka minne huku akitaka kama
hawana mashtaka waachiwe.
Tangu atoe kauli hiyo wakati wa
futari ya mwezi wa ramadhan aliingia matatani na kutakiwa kufika ofisi ya DCI
kwa ajili ya mahojiano na hadi sasa amekwishafika hapo mara tatu.
NA MWANDISHI WETU
No comments:
Post a Comment