'MACHINGA'wapewa siku 3 kwa hiari yao kupisha mradi ujenzi wa barabara za juu (flyover) Ubungo mataa...#share
WAFANYABIASHARA wadogowadogo maarufu ‘Machinga’ wamepewa siku
tatu kuondoka eneo la Ubungo mataa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar
es Salaam ili kupisha mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Flyover) unaotarajiwa kuanza Septemba
3 mwishoni mwa wiki hii.
Kushoto ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob na kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Kayombo wakizungumza na wafanyabiashara 'Machinga' leo Ubungo jijini Dar es Salaam
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John
Kayombo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzungumza na
wafanyabiashara hao juu ya kuondoka katika eneo hilo, alisema watatakiwa kuhama
kuanzia jumamosi mchana kwenda katika soko la mwasiliano (Simu 2000).
“Maagizo ambayo tumekuja kuyatoa hapa kwa wafanyabiashara
wadogo wadogo maarufu kama ‘Machinga’ ni kuja kuzungumza nao kistaarabu
kuwaomba sasa wapishe eneo la mradi wa Ubungo flyover,” alisema Kayombo.
Aidha alisema wakandarasi anataka kuanza ujenzi wa mradi huo
na taratibu tayari zimekwisha kamilika kwani walishindwa kuanza kazi kutokana
na kwamba Machinga walikuwa katika eneo la mradi.
Alibainisha kwa kuwa wamekwisha zungumza nao wamekubali
kupisha eneo kwa hiari yao kutokana na faida za mradi huo huku akieleza
kuwaonesha eneo zima la ujenzi unapoishia ili watakaopenda kuendelea kukaa
kando ya barabara wajue pakuweka bidhaa zao nje ya mradi unapoishia.
Meya wa Manispaa hiyo Boniface Jacob alisema kuwa mradi huo
ulitakiwa kuaza tangu Maei 22 mwaka ambapo wakandarasi waliopewa mradi huo
wanazaidi ya siku 100 wakati mradi mzima ulitakiwa kukamilika ndani ya siku 980
hivyo siku zilizobaki ni takribani 818.
Alibainisha kuwa alifanya jitihada za kuzungumza na serikali
paomoja na Tanroad ili kuhakikisha wafanyabiashara hao wanaondolewa kitarabu
kwani kungetumika mabavu hata thamani ya mradi wenyewe ingeshuka.
Aidha alisema kuwa kupitia ofisi ya Mkurugenzi kumeandaliwa
utaratibu mzuri utakaotumika kuwahamishia katika soko la mawasiliano na kueleza
kuwa waliolengwa ni zaidi ya wafanyabiashara 2000.
Alisema watapewa stika maalumu zitakazowatambulisha na
kupatiwa maeneo ya kufanyia biashara zao na kwamba hawataruhusu wasiohusika
kupatiwa eneo.
Pia alisema kutokana na mradi huo kumetoakea fursa za ajira
zaidi ya 1000 pamoja na mamantilie kupatia maeneo maalumu ambayo watajengewa
vizimba kwa ajili ya kutoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi ambao watakuwa
katika shughuli za ujenzi wa barabara hiyo.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment