LHRC IMEZINDUA RIPOTI KUHUSU HAKI YA KUFANYA KAZI NA BIASHARA NCHINI ILIYOSHEHENI UKIUKWAJI ...#share
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezindua
Taarifa ya Haki za Binadamu na Biashara ya mwaka 2016 huku kikibainisha
taarifa hiyo imesheheni ukiukwaji mkubwa wa haki hizo kwenye masuala ya haki ya
kufanya kazi, umiliki wa ardhi, usawa wa kijinsia, pamoja na kampuni kukiuka
haki za binadamu.
Akizindua taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
Mtendaji wa kituo hicho Dk. Hellen Kijo Bisimba alisema tafiti ilifanyika
katika mikoa 14 huku akibainsha inaonyesha asilimia 62.18 ya wafanyakazi hawana
mikabata, asilimia 61.60 hawana nakala za mikataba huku asilimia 38.40
pekee wakiwa nayo ikiwa imeandikwa.
“ Ripoti inabainisha wafanyakazi wengi hawana mikataba ya
ajira wengi wao wanafanya kazi bila kupata haki ya msingi ikiwemo ya kunyimwa
kupewa nakala za mikabata yao,’’ alisema Dk. Bisimba.
Dk. Kijo amesema imebainika makampuni hayapeleki michango ya
wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mujibu wa sheria za kazi na
kwamba asilimia 45.85 wanalipwa muda wa ziada huku asilimia 54.15
wakinyimwa stahiki hiyo.
Amesisitiza kuwa wafanyakzi waliohojiwa na watafiti wa LHRC
walibainisha kuwa asilimia 53.01 hakuna matawi ya vyama vya kutetea wafanyakazi
makazini ila asilimia 35.81 walisema vyama hivyo havina uwezo wa
kuwakilisha vyema.
Ameoongeza kuwa katika suala la umiliki wa ardhi tafiti zinaonyesha
asilimia 50 ya ardhi inayomilikwa na wawekezaji haijaendelezwa na kwamba
vijiji vingi havina mpango madhubuti wa matumizi wa rasilimali hiyo.
Amefafanua kuwa takwimu zinabainisha wanawake hawana
kipaumbele cha kuapata ajira kwenye makampuni ukilinagnisha na wanaume ambapo
asilimia 12.3 hawana ajira huku wanaume ikiwa asilimia 8.5 wana changamoto
hiyo.
Pia alisema sekta ya viwanda imeonekana kuwapendelea zaidi
wanaume kwa asilimia 71.92 na wanawake ni asilimia 28.08 ya waliohojiwa
wakiwa katika kazi.
Aidha, amesema kundi la watoto limeonekana kuingizwa kwenye
ajira za utotoni kinyume na sheria za nchi ambapo asilimia 70 ya watoto
walibainika kufanya kazi kwenye mashamba.
Katika hatua nyingine, amesema ripoti hiyo inaonyesha
ukusanyayaji wa mapato ya ndani kwa mwaka umeongezeka hadi kufikia Sh trillioni
10.87 mwezi Julai wa mwaka huo.
Dk Kijo alisema makampuni yalionyesha uwajibikaji kwa
jamii kwa kushiriki uchangiaji wa madawati katika sekta ya elimu nchini.
Wakati huo huo, Dk Kijo amesema mwezi Juni mwaka jana
wafanyakazi 2,464,399 walisajiliwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii
ukilinganisha na mwaka 2015 walisajiliwa 2,142,350.
Na Hussein Ndubikile
No comments:
Post a Comment