mAHAKAMANI kISUTU: Video QueeN Agnes 'Masogange' azidi kubanwa matumizi dawa za kulevya...Mkemia Mkuu wa Serikali aushtukia mkojo wake kuwa na chembechembe ya dawa hizo...#share

OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali imewasilisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu taarifa inayoonesha kuwa sampuli ya mkojo wa Video Queen, Agnes Gerald "Masogange" una chembechembe za dawa za kulevya.


Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema leo kwamba pingamizi la upande wa utetezi kuwa fomu zilizopelekwa kwa mkemia hazikufata sheria limetupiliwa mbali na mahakama imepokea taarifa hiyo ambayo itatumika kama ushahidi.

Amesema shahidi wa kwanza ambaye ni Elia Mulima anahaki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti mahakamani. Pia amesema Polisi walipeleka maombi kwa mkemia wa serikali na kwamba ni wazi mshitakiwa alienda kwa mkemia na askari wawili na kumpatia kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo.

Mpelelezi kutoka Ofisi ya Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, WP Judith ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa alishuhudia Masogange akitoa sampuli ya mkojo kwa kuwa alisimama mlangoni.

Amedai kuwa alipewa chupa ya plastiki yenye namba ya maabara 446/2017 na kumuelekeza Masogange jinsi ya kufanya ambapo alipata sampuli ya mkojo huo. 

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, shahidi huyo alidai kuwa Februari 15, mwaka huu aliitwa na Kaimu Mkuu wa Upelelezi, Ramadhan Kingai amchukue mshitakiwa Masogange na kumpeleka kwa Mkemia wa Serikali.

Amedai baada ya kuchukua aliongozana na Askari Polisi, Sospeter kwenda kwa mkemia na kwamba saa 7 mchana walifika. "Lengo la kumpeleka kwa mkemia ni kupimwa sampuli ya mkojo kwa kuwa alituhumiwa kwa kutumia au kusafirisha dawa za kulevya," alidai Judith.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza alimtaka shahidi huyo kueleza alikabidhiwa na nani chupa na kwamba mkojo ulikuwa na rangi ambapo shahidi huyo alieleza kuwa ulikuwa na rangi ya njano mpauko. Hakimu Wilbard Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 31, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search