Mbunge wa Zamani wa Ukonga na Segerea Dk. Mahanga akamatwa na Polisi kwa amri ya Mahakama...#share
ALIYEKUWA Mbunge wa Ukonga na Segerea kwa , Dk Makongoro
Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na
kufikisahwa mahakamani.
Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa
mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba
Msemakweli Sh14 milioni.
Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada
ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja
kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.
Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye
shahada za udaktari wa kughushi.
Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6
milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.
Na Mwandishi Wetu.
No comments:
Post a Comment