Waumini wa Dini ya Kiislam watakiwa kusherehekea Sikukuu ya Eid Haji kwa Amani na Upendo...#share
WAKATI Waumini
wa Dini Kiislam nchini wakiungana na wenzao Duniani
kesho wakiwa wanasherekia sikuku ya Eid Haji, wametakiwa
kusherekea sikuku hiyo kwa kuhakikisha wanadumisha amani na upendo katika
jamii.
Pichani ni Kiongozi wa Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheria Tanzania, Sheikh Hemed Jalala
|
Pia wametakiwa
kuhakikisha wanafanya mambo ya kumpendeza mungu katika sikuku hiyo na kuacha
kufanya mambo ya kumchukiza Mungu .
Wito huo umetolewa leo
Jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheria Tanzania,
Sheikh Hemed Jalala wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia sikuku
hiyo, ambapo amesema sikuku hii ni nembo kubwa kwa waislam ,basi hawana budi
kuhakikisha wanaijenga jamii isiyokuwa na aina yoyote ya vurugu.
“Nawaomba waislam
tutumie sikuku hii katika kujitafakari na kuhakikisha tunailinda amani yetu
hapa nchini Tanzania ,kwa kuleta umoja na mshikamano huu kwetu,na tusikubali
kufarakana katika jamii”Amesema Sheikh Jalala.
Kiongozi huyo wa kiroho
ameenda mbali kwa kuwataka waislam kututumia sikuku hii muhimu kwa kusherekea
kwa kufanya maasi jambo analodai linakwenda kinyume na sheria za
dini ya kiislam.
“Mtu anayemkosea
Mungu Siku ya sikuku ya Eid mtu huyu ni kama amemkosea mungu siku ya
kiama”amesema Shekh Jalala.
Sheikh Jalala pia
ameitaka serikali kuhakikisha wanatumia rasilimali zilizopo hapa katika nchi
za Afrika zitumike katika kutatua tatizo la ajira.
“Bara la Afrika bado
linalinasumbuliwa na matatizo mengi sana ikiwemo umasikini,bado linasumbuliwa
na maradhi bado Afrika inasumbuliwa na njaa,basi tunawaomba viongozi wa Afrika
kutumia rasilimali zilizopo katika maneno yetu zitumike katika kutatua matatizo
ya ajira ili ipatikane jamii yenye kufanya kazi”ameendelea kusema Sheikh
Jalala.
Hata Hivyo,Sheikh Jalala
amewataka pia waislam ambao walikwenda kufanya Hija kutumia njia hiyo katika
kuhakikisha wanaijenga jamii nzuri isiyo kuwa na aina yoyote ya fujo na
mfarakano katika jamii.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment