MVURUGANO: Mwanachama TLS alaani vikali Uongozi kuitisha mgomo wa siku mbili Mahakamani....Autaka kuacha kulitumia Baraza lao Kisiasa na Kiharakati.....#share
SIKU moja baada ya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa
Tanganyika (TLS) kuitisha mgomo wa siku mbili kwa wanachama wake nchini wa kutohudhuria
katika Mahakama pamoja na Mabaraza ya aina zote, Mkurugenzi Mtendaji wa Smile
Stars Attorneys na Mwanachama wa TLS Leonard Manyama amelaani kitendo hicho na
kuutaka viongozi wao kutolitumia Baraza kwa maslahi yao kisiasa.
Jana BARAZA la Uongozi la TLS kupitia Rais wao Tundu Lissu
liliwataka Mawakili wote wanachama wa chama hicho kususia kuhudhuria katika
Mahakama pamoja na Mabaraza ya aina zote kati ya kesho na kesho kutwa ( Agosti
29 hadi 30 mwaka huu).
Lissu alisema lengo la mgomo huo ni kuunga mkono mawakili wa
IMMMA Advocates waliounguliwa na Ofisi zao kwa mlipuko wa mabomu ili kuonyesha
kutokubaliana kwao na vitendo vya kihalifu vya kuwashambulia mawakili hao.
Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari, Manyama
amewataka wanachama wasikubali chama hicho kutumiwa kisiasa na kiharakati.
“Kitendo kile kimefanywa na wahalifu wenye nia ovu ambao vyombo
vya dola vitawashughulikia, kufanya mgomo ni kuumiza wanachi wengine wasio na
hatia kwa sababu tu ya kikundi kidogo cha wahalifu,” amesema Manyama.
Aidha amesema badala ya kufanya mgomo huo wanatakiwa kuacha
vyombo vya dola kufanya uchunguzi ili kubaini wahalifu hao huku akieleza kuwa
itakuwa ni kitendo cha ajabu kama mawakili watatekeleza agizo hilo wakati
vyombo hivyo vikendelea na uchunguzi.
Ameendelea kusema kuwa uhalifu huo uneweza kutokea mahali
popote ambapo alitoa mfano kwa tukio la uhalifu lililowahi kutokea katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam lakini hakuna
tamko la jinsi hiyo lililotolewa na TLS huku tukio hilo pia likiwa na viashiria
vya kuingilia uhuru wa Mahakama na mawakili.
Amesesitiza kwa kuwataka Mawakili kuachana na mgomo huo ili
kutoathiri wananchi walio wengi wanaohitaji msaada wao wa kisheria. Amewataka wananchi
wenye ushahidi wa tukio hilo la shambulio kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola
ili kuwakamata watekelezaji wa shambulio hilo.
Aidha amelitaka Baraza la Uongozi wa TLS kuacha kutoa matamko
ambayo yanaweza kujenga uadui baina ya wanachi na serikali kwani kwa kauli zile
zianafanya wananchi kuamini kuwa vyombo vya dola ndiyo vilivyohusika.
Jana Rais Lissu alisema kuwa waliotekeleza ni kikundi cha
watu ambao walikuwa wamevalia sale za Jeshi la Polisi ambapo Manyama amefafanua
kuwa hata majambazi wanaweza kuvaa sale hizo ili kufanya uhalifu kwa urahisi.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment