sPORTS nEWS: Haji Manara amnyooshea Mikono Kamsoko wa Yanga....Adai si mchezaji watanzania....#share
OFISA Habari wa Klabu ya Simba Haji Manara amedai kuwa wa
Kimataifa wa Klaby ya Yanda Mzimbabwe Thabani Michael Kamusoko hana hadhi ya kucheza
mpira katika vilabu vya Tanzania.
Manara amesema hayo
kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba anatakiwa
kucheza ulaya kutokana na mchezaji huyo kuwa na jitihada pamoja na umahiri mzuri
wa kusakata kabumbu uwanjani.
"Huwa sifichi mahaba yangu kwa mchezaji anayenivutia
uwanjani hata kama anachezea klabu nisiyoishabikia. Scara Kamusoko hapewi
heshima anayostahili nchi hii. 'Level' yake ni kucheza Ulaya", ameandika
Manara.
Kamusoko ni mmoja miongoni mwa wachezaji wa klabu ya Mtaa wa
Twiga na Jangwani Yanga ambao wamekuwa wakionyesha kiwango kizuri na kuisaidia
klabu katika mashindano mbalimbali.
Aidha mchezaji huyo ameweza kuonyesha kiwango kizuri jana katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya
Ligi Kuuu Tanzania Bara dhidi ya Lipuli FC ambapo klabu hizo zilitoka sare ya mabao 1-1 katika mchezo ulipigwa
katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment