nEW: Lissu akamatwa na polisi akitoka Mahakamani Kisutu.....Ofisa Habara wa Chadema Tumaini Makene athibitisha.....#share

*Attn; Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Lissu amekamatwa na polisi*

Tumetoka Mahakama ya Kisutu muda huu ambapo Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lissu alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi (uchochezi one) lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili Yericko Nyerere hapa hapa Kisutu.

Wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likawa blocked na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police.

Wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Police.

*Makene*

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search