Zitto asikitishwa na Anguko la mauzo ya bidhaa nje, adai hali hiyo kutufanya Tegemezi...#share
MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama
cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amesema kuwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi hususan
chakula yanazidi kushuka huku uingizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ukipanda hasa
kipindi hiki nchi inapopambana na ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Zitto amesema hayo kupitia ukurasa wake wa facebook na Amebainisha
kwa kusema kuwa anguko hilo, linatufanya nchi kuzidi kuwa tegemezi.
“Uagizaji wa bidhaa za chakula kutoka nje umeongezeka kwa 14%
ndani ya mwaka mmoja wa Mei 2016 mpaka Mei 2017, ambapo Tanzania ilitumia dola
480 milioni kuagiza vyakula kama sukari, nafaka na mafuta ya mawese. Tumekuwa
tegemezi zaidi, tunauza bidhaa kidogo zaidi nje ya nchi, na tunanunua bidhaa
zaidi kutoka nje", amesema
Zitto Kabwe.
Mbunge huyo amendelea kusema kuwa fedha ambayo serikali
inapoteza kwa anguko la mauzo ya bidhaa ndani ya miaka miwili ni nyingi, ambayo
ingeweza kununua ndege 23 za aina ya bomberdier Q400.
“Wakati Serikali inaimba viwanda, mauzo ya bidhaa zitokanazo
na viwanda kwenda nje ya nchi yetu yameshuka sana, mwaka unaoishia Mei, 2016
Tanzania iliuza nje bidhaa za viwanda za thamani ya dola 1.5 bilioni. Mwaka
mmoja baadaye Tanzania imeuza nje bidhaa za viwanda za thamani ya dola 0.8 bilioni
tu. Anguko la mauzo nje la takribani dola 700 milioni sawa na thamani ya Ndege
23 za Bombadier Q400", aliandika Zitto Kabwe
Na Mwandishi Wetu





No comments:
Post a Comment