sPORTS nEWS: Yanga yaanza kwa kuchemeea VPL, yashindwa kufurukuta mbele ya Lipuli...#share

KLABU Yanga imevutwa shati na klabu ya Lipuli kwa kutoka bao 1-1 katika mchezo wea ligi kuu Tanzania Bara iliyomalizika hivi punde katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


Mabao hayo yote yalipatikana kipindi cha kwanza ambapo Timu ya Lipuli ilikuwea ya kwanza kupata goli dakika ya 44 kupitia kwa Seif Abdallah huku Donald Ngoma akiisawazishia Yanga dakika ya 45’.

 Kikosi cha Lipuli kilichoanza katika mchezo huo kilikuwa kama ifuatavyo, Mohammed Yusuph, Samweli Nkomela, Paul Ngalema, Novatus Lufunga, Ahsante Kwasi, Hamad Manzi, Salum Machaku, Omega Seseme, Jerome Lalembe Seif Abdallah, Shaban Ada.

Huku kikosi cha Yanga kikianza na wachezaji, Youthe Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vicent, Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Rafael Daudi, Thabani Kamusoko, Ibrahimu Ajibu, Donald Ngoma, Emanuel Martin




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search