nEWS: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yalaani shambulio katika Ofisi za IMMMA Advocates....Yalitaka Jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wa tukio hio...Pia waitaka TLS kusitisha mgomo wa siku 2 kesho na kesho kutwa....#share
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imelaani
kitendo cha kupigwa bomu Jengo la Ofisi
za Wanasheria wa IMMMA zilizoko Barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es
Salaam kilichotokea usiku wa kuamkia Agosti 26 mwaka huu.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya jengo hilo kuvamiwa
na kulipuliwa na kitu chenye mshindo mkubwa kinachodhaniwa ni bomu na kusababisha
uharibifu mkumbwa huku ikiripotiwa hakuna kitu kilichochukuliwa.
Taarifa iliyotumwa leo kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti wa
tume hiyo Bahame Nyanduga, amesemna THBUB imesikitishwa na kitendo hicho na
kwamba kinaashiria uhalifu wenye nia ya kutisha wanasheria wasitekeleze
majukumu yao ya kisheria ya kutetea wateja wao.
Nyanduga amesema tume hiyo inasisitiza kuwa dhana ya utawala
bora inategemea utawala wa sheria, ambao utaathirika iwapo wanasheria
watatishwa na matukio kama ya kupigwa mabomu au vitendo vinginevyo
vitakavyowanyima uhuru wa kufanya kazi zao.
Amesisitiza kuwa tume inalitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha
linakamilisha upelelezi wa tukio hilo na kuwapeleka wahusika katika vyombo vya
sheria.
Aidha, ameutaka uongozi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika
(TLS) kusitisha tamko lililowataka Mawakili kususia kuhudhuria Mahakamani na
Mabaraza ya aina zote kwa siku mbili kwani mgomo huo hautakuwa na maana kwa
kuwa vyombo vya usalama vimeshaanza kufanya uchunguzi.
Pia amesema ni vyema
TLS ikasitisha mgomo huo kwani utawaathiri wateja wao ambao hawahusiki na tukio
la kupiga bomu.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment