nEWS: Serikali yawataka vijana kuacha kulalamika...Yawahimiza kuchangamkia fursa kujikwamua kiuchumi....#share
SERIKALI imwataka vijana kuacha tabia ya kulalamika badala
yake wajikite katika kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ili kujikwamua
kiuchumi huku ikibainisha inaendelea na hatua za uanzishwaji wa Baraza la
Vijana la Tanzania.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Bunge,
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama wakati wa Ufunguzi
wa Mkutano wa Vijana wa Kitaifa wa Afya na Maendeleo.
Amesema vijana wengi wamejenga utamaduni wa kulalalmika hali
ya ngumu ya maisha pasipo kutimiza wajibu wao kwa kuhangaikia fursa kuzifanyia
kazi huku akisisitiza endapo watazifanyia kazi zitawasaidia kujikwamua
kimaisha.
''Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na jitihada za
kuwasaidia vijana kinachotakiwa vijana waache kupiga kelele bila kutimiza
wajibu wao fursa zipo nyingi zinazoweza kuwawezesha kiuchumi,'' alisema
Jenista.
Waziri Jenista amesema vijana wanatakiwa kutumia akili zao
kama mtaji kupambanua mambo na mazingira yanayowazunguka kujiletea maendeleo.
Amesisitiza kuwa Sheria namba 12 ya mwaka 2015 inayohusiana
na uundwaji wa baraza hilo ilikwishatungwa kanuni huku akiongeza lengo la kuwa
na chombo hicho ni kuwaleta vijana pamoja na Serikali yao.
Amefafanua kuwa katika kuhakikisha kundi hilo linajikwamua
kiuchumi vijana 2,500 wameanza kupatiwa mafunzo katika kiwanda cha Tuki Garmert
kilichopo Ubungo ya utengenezaji wa nguo zitakazouzwa nje ya nchi.
Pia amesema vijana 1,000 wanaendelea kupatiwa mafunzo ya
uongezaji thamani wa bidhaa za ngozi huku 13,400 waliopo kazini wakipewa
mafunzo hayo ambapo waemilishaji rika 60 watasambazwa mikoani kuwaelimisha
vijana.
Amewashauri vijana kupima virusi vya Ukimwi kwa hiari katika
vituo vinavyotoa huduma hiyo ili kutambua hali za afya zao.
Kwa upande wake MKurungenzi wa Shirika la Save the Childern nchini
Peter Wash amesema mkutano huo utasaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa changamoto
zinazowakabili vijana zikiwemo za ukosefu wa ajira, magonjwa na uchangamkiaji
fursa.
Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Kuratibu na Kudhibiti Ukimwi
nchini (TACAIDS) Jumanne Isango amewataka vijana kuendelea kufanya jitihada za
kujiletea maendelea na kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwani kundi
hilo linaongoza kwa maambukizi hayo.
Na Hussein Ndubikile
No comments:
Post a Comment