News(+Video): Tumaini Makene Kathibitisha kukamatwa kwa Mbunge kijana wa Chadema MHE.Esther Bulaya jioni ya Leo.. #share



Kuna taarifa zilizosambaa sana mtandaoni jioni hii za kumuhusu Mbunge wa Bunda Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ester Bulaya kukamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Rorya katika Mkoa wa Mara akiwa katika majukumu ya kichama.


Akithibitsha Taarifa hiyo, msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene, amesema Esther amekamatwa akiwa akiwa katika Hoteli aliyofikia Tarime ambako alikwenda kwa ajili ya shughuli za kichama... "Ni kweli tumepata taarifa muda sio mrefu kwamba Mbunge wetu Jimbo la Bunda Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa Hotelini kwake, Tarime. Alikuwa katika shughuli za kichama akiwa kama Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search