sPORTS nEWS: Zama za ubabaishaji TFF sasa kwisha, Rais Karia aanza kwa kushusha rungu kali Bodi ya ligi kwa kuvurunda.....#share

KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred
Kidao amesema kuwa ameagizwa na rais wa Shrikisho hilo, Wallace Karia
kumwandikia barua Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi ili kuwaadhibu viongozi wa Bodi
ya Ligi waliohusika na kupanga ratiba.
Pichani ni Mtendaji
Mkuu wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura.
Kumekuwa na malalamiko kutokana na Bodi hiyo kupanga ratiba
ya ligi ambapo walishindwa kuzingatia kuwa kuna michezo ya kimataifa ambayo
itahusisha timu za taifa jambo ambalo limesababisha baada tu ya mchezo mmoja
tu, ligi hiyo ikapanguliwa tena.
“Nimeagizwa na rais nimwandikie barua mtendaji mkuu wa bodi
ya ligi ili aweze kuwachukulia hatua viongozi wa bodi hiyo waliohusika na
kupanga ratiba hii pamoja na kwamba walikuwa na kalenda lakini bado wamekosea,”
alisema Kidao.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura ambaye sasa atakuwa na jukumu la kuchukua hatua kwa wasaidizi wake.
No comments:
Post a Comment