mAHAKAMANI kISUTU: Baada ya Mahakama jana Kuarifiwa kuwa Bilionea Manji ana vyuma kwenye moyo....Leo yaelezwa Sethi naye ana 'Puto' tumboni mwake...#share

MAHAKAMA ya Hakimu
Mkazi Kisutu imeelezwa na upande wa utetezi kuwa Mmiliki wa Kampuni ya kufua
umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi amewekewa ‘Puto’ tumboni kutokana na
ugonjwa unaomkabili hivyo asipohudumiwa inavyotakiwa anaweza kupoteza maisha.
Mbali ya Seth, mwingine
ni Mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka
12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya TSh
309,461,300,158.
Wakili wa utetezi,
Joseph Mwakandege amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mteja wake
Seth anatakiwa apelekwe Hospital ya Taifa Muhimbili lakini hadi sasa
hajapelekwa na ni dhahiri upande wa mashtaka umedharau amri mbili za Mahakama.
”Ugonjwa uliosababisha
Seth atakiwe kwenda Muhimbili ni baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa ambapo
tumboni kwake kumewekwa Balloon ‘Puto’ hivyo asipohudumiwa ipasavyo inaweza
kusababisha kifo, naomba mshtakiwa apelekwe Muhimbili kwa sababu ni Hospitali
ya juu na yenye vifaa na watalaamu wa kutosha“ amesema Mwakandege.
Akijibu hoja hizo,
Wakili wa Serikali Vitalis Peter amedai kuwa Magereza hawapangiwi wampeleke
wapi mshtakiwa ambaye ni mgonjwa bali wana utaratibu, Hospitali na watalaam
wao.
”Mshtakiwa alianza
kupelekwa Hospital ya Magereza, kisha Hospital ya Amana ambapo alikutana na
daktari mtalaam kutoka Muhimbili na aliweza kumuangalia afya yake, hivyo hoja
ya kwamba hatujatekeleza amri ya Mahakama sio kweli.” Peter
Baada ya kusema hayo,
Hakimu Shahidi amesema alishatoa amri mara mbili kwamba Seth akatibiwe
Muhimbili na kusisitiza akatibiwe ”Nasisitiza tena, mshtakiwa
akatibiwe Muhimbili, sioni kama kuna sababu ya kulumbana, kesi imeahirishwa
hadi September 14, 2017.”
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment