tETESI zA uSAJILI uLAYA: Wakati dirisha la usajili likielekea kufungwa Wenger hamtaki Mustafi...Adumu na Arsenal kwa miezi 12..... Awekwa sokoni....#share
KLABU ya Arsenal huenda ikaachana
na beki wake Shkodran Mustafi kabla ya dirisha la usajili la msimu huu wa
kiangazi kufungwa Alhamisi ya wiki ijayo.
Kwa mujibu wa Daily Mail Online imearifu
kuwa Arsene Wenger amefungua milango ya kumuuza mchezaji huyo amabaye amedumu
na klabu hiyo kwa mwaka mmoja tangu aliposajiliwa msimu uliopita.
Aidha taarifa zinaeleza kuwa Juventus
na Inter Milan wameonyesha kumhitaji mchezaji huyo. Klabu ya Inter Milan tayari imeshamuulizia mchezaji huyo huku Juventus pia
wakiwa wakifuatilia kwa karibu uwezekano wa kumsajili.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujeruman alijiunga na Washika
Mtutu hao wa London msimu uliopita wa kiangazi kwa pauni milioni 35 lakini kwa
sasa klabu hiyo iko tayari kuachana naye.
Arsenal wanataka kurudisha kiasi hicho cha fedha walichotumia
kumnunua Mustafi hivyo kiasi cha ada ambacho kitakaribiana na pauni milioni 35
kikitolewa na timu yoyote inayomhitaji klabu inaweza kumuuza.
Mustafi alionyesha kiwango kizuri
katika miezi ya mwanzoni msimu uliopita, lakini kuelekea mwishoni mwa msimu huo
kiwango chake kilianza kilishuka na ilisababishwa na kuwa majeruhi.
Na Mustafi siyo mchezaji pekee
anayehusishwa kuihama Emirates msimu
huu wa kiangazi lakini pia Alex
Oxlade-Chamberlain huenda akaihama klabu hiyo.




No comments:
Post a Comment