Baada ya Kukamatwa na Jeshi la Polisi, Zitto Asema Nchi Tumewakabidhi Washamba...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share

WAKATI taarifa zikieleza kuwa Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amekamatwa na jeshi la Polisi kwa agizo la Katibu Mkuu wa Bunge Dk . Thomas Kashililah.
Mbunge huyo ameibuka katika mitandao ya kijamii na kudai kuwa nchi imekabidhiwa kwa kwa washamba. Zitto ameandika hivi.

“Tumekabidhi nchi Kwa washamba na malimbukeni wa madaraka. Mihimili karibu yote ya dola letu inaongozwa na malimbukeni. ' wajanja ' wanalamba miguu ya washamba ili kuishi tu. Werevu wananyamazishwa, wanaitwa si Wazalendo,”.

“Wanapangiwa mauaji. Nchi imewashinda. Anguko kubwa la uchumi laja sababu ya maamuzi ya kishamba na kukosa maarifa. Hata hivyo watabaki werevu kadhaa na watarejesha nchi yetu kwenye mstari,” amesema Zitto kwenye ukurasa wake wa Fecebook.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search