Mkutano wa ALAT Kufanyika Oktoba Mkoani Mbeya....Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share
JUMUIYA ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania
(ALAT) imesema Mkutano Mkuu wa jumuiya hiyo unatarajiwa kufanyika mkoani Mbeya
kuanzia Oktoba 2 hadi 5 huku ikibainisha Benki ya NMB imetoa Sh milioni 100 kwa
ajili ya kufadhili mkutano huo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar na Kaimu Katibu Mkuu wa ALAT,
Abdallah Ngobi wakati akipokea fedha za ufadhili wa mikutano kutoka kwa benki
hiyo.
Amesesema mkutano huo utashirikisha wajumbe 500
kutoka mikoa mbalimbali huku akisisitiza miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa ni
kuzishinikiza halmashauri zote kutenga fedha kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo
lengo likiwa kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
“ Ajenda mbalimbali zitajadiliwa zikiwemo za kuzihimiza
Halmashauri kuwa na utaratibu wa kuwa na maeneo yatayojengwa viwanda vidogo,
ufafanuzi wa utendaji kazi wa Wakala wa Barabara wa Mijini na
Vijijini (Tarura),” alisema Ngobi.
Amebainisha kuwa katika mkutano huo Halmashauri zitaelekezwa
jinsi ya kusimamia na kufanya kazi na Tarura hasa walengwa wakiwa wenyeviti wa
serikali hizo , watendaji ina mameya.
Amefafanua kuwa jumuia hiyo inapongeza utendaji wa Serikali
ya Awamu ya Tano kwa jinsi inavyoendesha nchi ikiwemo kusimamia ukusanyaji
mapato, kupambana na ufisadi, rushwa na uwajibikaji.
Ameipongeza na kuishukuru benki hiyo kwa msaada
huo huku akiiomba iendelee kuisaidia ALAT katika kufanikisha mambo mbalimbali
yenye manufaa kwa taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa benki hiyo,
Richard Makungwa amesema NMB inatambua mchango wa ALAT na kwamba katika
Halmashauri 185 imefunga mashine za kielektroniki 170.
Amesesma benki hiyo itaendelea kuifadhili ALAT na
kuweka wazi NMB ina kitengo maalumu cha kuwasaidia wafanyabiashara wadogo
wadogo kwa kuwapatia mikopo ya kupanua Biashara zao.
Na Hussein Ndubikile
No comments:
Post a Comment