Breaking: Nyumba ya Mbunge zitto Kabwe yaungua Moto...#share
NYUMBA ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) iliyopo Mwandiga, mkoani Kigoma yaungua moto muda huu.
Nyumba hiyo iko kiwanja kimoja na nyumba yake ya sasa imeteketea yote na chanzo chake hakijafahamika hadi sasa.
Msaidizi wa mbunge huyo, Nyembo Mustafa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hata hivyo Zitto hakuwa anaishi kwenye nyumba hiyo.
Amesema Zitto alihama kwenye nyumba hiyo baada ya kujenga nyumba nyingine kubwa kwenye kiwanja hicho hicho na iliyoungua ilikuwa ikitumika kwa dharura.
No comments:
Post a Comment