Mbivu Mbichi Kesi Matumizi Dawa za Kulevya ya Manji kujulikana Oktoba 6...Taarifa Zaidi na Matukio360..#share

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu kesi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji, October 6, 2017 baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wake wa mashahidi saba.

Hatua hiyo inatokana na Wakili wa Manji, Hajra Mungula kumueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwamba wamefunga ushahidi wao wa mashahidi saba ambapo baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha amesema kutokana na kufungwa ushahidi huo anatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo, October 6, 2017.

Awali, Manji kupitia Wakili wake Mungula, aliiambia Mahakama hiyo kwamba angekuwa na mashahidi 15 lakini hadi leo September 26, 2017 ni mashahidi saba tu waliotoa ushahidi wao.

Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya February 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
Chanzo: Millard Ayo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search