Bunge Laibuka na Nyaraka Likifafanua Utata wa Fedha za Wabunge Milioni 43 za Matibabu ya Lissu..#share

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Septemba 24, 2017 limetoa ufafanuzi na uthibitisho wa risiti ya malipo ya fedha za wabunge milioni 43 kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu ambazo zilichangwa na wabunge na kulipwa hospitali ya Nairobi.

Bunge limelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa hospitali ya Nairobi mbaka jana ilisema haijapokea fedha hizo kutoka kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

"Ofisi ya Bunge inapenda kusisitiza kuwa fedha zilizochangwa na Wabunge kiasi cha Tsh. Milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mheshimiwa Tundu Lissu tayari zimetumwa katika Akaunti ya Hospitali ya Nairobi anakopatiwa matibabu. Fedha hizo zimetumwa kupitia Benki kuu ya Tanzania (BOT) ambapo kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BOT kwa siku hiyo ilikuwa ni sawa na Shilingi ya Kenya 1,977,120.58." ilisema taarifa ya Bunge 

Taarifa hiyo ya Bunge iliendelea kusisitiza kuwa walituma fedha hizo Septemba 20, 2017 
"Kiasi hicho cha Fedha kilitumwa siku ya tarehe 20 Septemba, 2017 kwenda Benki ya Barclays, Tawi la Hurlringham, Akaunti Namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association" 

Septemba 22, 2017 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alisema kuwa mbaka siku hiyo anatoa taarifa mbalimbali kuhusu Tundu Lissu fedha ambazo wabunge walikuwa wamechanga kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu zilikuwa hazijafika Hospitali Nairobi Kenya, lakini siku moja baadaye Bunge lilitoa taarifa na kusema walikuwa wameshatuma fedha hizo toka Septemba 20 mwaka huu, baadaye zikawepo taarifa kutoka hospitali ya Nairobi kuwa bado hawajapata fedha hizo kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search