CWT Geita kimewatangaza Mashujaa wa Elimu, Wanafunzi walifariki kwa ajali Ziwa Victoria..

Na,Denice Simba
Chama cha walimu CWT tawi la Geita kimewatangaza wanafunzi watatu waliopoteza maisha katika ziwa Victoria wakati wakivuka kutoka shuleni kuwa mashujaa wa elimu


Wanafunzi hao wa Shule ya msingi Butwa walipoteza maisha katika ajali ya majini iliyotokea mwezi juni mwaka huu baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kupinduka na kuzama

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake,Katibu wa CWT wilaya ya Geita Mwl. John Kafimbi amesema Chama chake kinafanya maandalizi ya kujenga makaburi ya wanafunzi hao kama sehemu ya makumbusho
Aidha, Mw. Kafimbi ameeleza kuwa vifo vya watoto vimekuwa chachu ya maboresho kat ka sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na mipango ya kujengwa shule mpya ya msingi katika kisiwa cha Butwa-Lulegea.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search