DC Hapi Akerwa..Apiga Marufuku Bomoabomoa..Soma Habari Kamili na Matukio360...#share
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amepiga marufuku ubomoaji wa nyumba bila idhini yake.
Pia, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata madalali wa Mahakama wanaotumiwa kubomoa nyumba za wananchi bila kupata kibali kutoka kwake.
Amesema hayo leo Jumatano, alipozungumza na wananchi wa Kata ya Kunduchi alipotembelea eneo hilo akiwa ziarani kikazi kusikiliza kero za wananchi na kukagua miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Soko la Samaki.
Marufuku hiyo imetolewa baada ya Diwani wa Kunduchi, Michael Urio kutoa kero kwamba kuna watu wamevunjiwa nyumba pasipo viongozi wa maeneo husika kushirikishwa.
Hapi amesema kumekuwa na kesi nyingi ofisini kwake kuhusu kubomolewa
nyumba na watu aliowaita matapeli na kwamba, kuanzia sasa hakuna atakayebomoa bila ya yeye kujua.
Amesema lengo ni kuhakikisha nyumba zinazobomolewa zimeainishwa na
Mahakama kwa kuwa madalali wengine wanaghushi hukumu.
"Ni marufuku mtu kuvunja nyumba bila mimi na vyombo vyangu kuwa na taarifa. Hatuwezi kuvumilia huu mchezo, kama kuna dalali amekwenda kuvunja nyumba ambayo haijaainishwa kwenye hukumu ya Mahakama akamatwe mara moja," amesema.
Hapi amesema, "Zipo kesi zimetokea kwenye wilaya yetu, wale madalali wamekuwa wakivunja nyumba ambazo hazijaainishwa, Mahakama inasema nyumba namba 13 wao wanavunja nyumba namba 23," amesema.
Katika hatua nyingine DC Hapi amechoma nyavu haramu zenye gharama ya shilingi milioni 20, huku akisitiza uvuvi unao fuata sheria, na kusisitiza kuwa kwa kushirikiana na ubalozi wa Sri Lanka kupitia balozi wake Lal Silva amehaidi kuisaidia Tanzania vifaa vya kisasa vya uvuvi na kutoa mafunzo kwa wavuvi.
" Niwaombe wavuvi mjiunge katika vikundi ili muweze kufikiwa vizuri na fursaza kiuchumi na tuondokane na uvuvi uliopitwa na wakati wa kutumia vifaa duni, tujiandae mapinduzi ya uvuvi wa kisasa yanakuja, nashukuru serikali ya Sri Lanka wako tayari kutusaidia nitatuma maombi rasmi na tukikutana kupitia vikundi vyenu tutaangalia namna ya kuzitumia fursa hizo" Alisema
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment