Jumia Tanzania waja na Mfumo Mpya wa Manunuzi kwa Njia ya Mtandao...#share



Kampuni inayojihusisha na kutoa huduma ya manunuzi ya bidhaa kwa njia mtandao  ya JUMIA TANZANIA imeboresha huduma zake kwa kuja na mfumo mpya ujulikanayo kama  CASH ON DELIVERED [COD]ambayo itawawezesha wateja wanaogiza bidhaa kupuitia tovuti ya Jumia Tanzania kulipia bidhaa mara baada ya bidhaa hizo kuwafikia.


Meneja masoko wa kampuni ya Jumia Tanzania, Albany James  akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam meneja masoko wa Jumia Tanzania, Albany James amesema kuwa mfumo huo mpya utawajengea uaminifu wateja wanaonunua bidhaa kupitia mtandao kujenga uaminifu kwa huduma zote za manunuzi wanazozifanya kwa njia ya mtandao.


‘’jumia Tanzania tunayo furaha kuwajulisha wateja wetu wote kwamba hivi sasa wanaweza kulipia bidhaa zao wanazozinunua kwa njia ya mtandao pindi bidhaa zinapowafikia na tumeona ni vyema kuwapa wateja wetu chaguo hilo kwa kulipia bidhaa baada ya kuziona kwa macho na kujiridhisha kwani huduma ya manunuzi kupitia mtandao ni ngeni kwa watanzania walio wengi jambo linalofanya engi wao kuwa na hofu na kudhani wanatapeliwa’’amesema James


Akizungumzia faida za mfumo huo mpya  James amesema mbali na mteja kuionana kujiridhisha na bidhaa aliyoiagiza kabla ya kufanya malipo pia mteja atapata fursa ya kuweza kubadilisha bidhaa endapo hatoridhika nayo na kumfanya mteja kuchagua kulipia fedha kwa njia ya mtandao ama pale bidhaa itakapomfikia.
 
“ningependa kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia ofa mbali mbali za manunuzi ya bidhaa kupitia tovuti yetu au mitandao ya kijamii ya Facebook,Twitter na Instagram lakini pia wafanyabiashara wa kitanzania kuhamia kwenye njia za mitandao ili kupanua wigo kwa wateja wao kuna faida nyingi za kujiunga na Jumia Tanzania ikiwemo kujiongezea wateja wengi tofauti na wale wanaotembelea maduka yao moja kwa moja’’ameeleza James.


Jumia Tanzania ambayo imeanza kazi zake rasmi hapa nchini miaka miwili iliyopita imefanikiwa kutanua wigo wa biashara za mtandaoni kwa kuwawezesha watanzania wengi kununua bidhaa mbali mbali kutoka katika maduka na kampuni mbali mbali kupitia mitandao jambo ambalo limekuza teknolojia hiyo ambayo inawapa urahisi wateja kununua bidhaa bila kuzifuata madukani.
 

Ofisa Mkuu wa Biashara Jumia Tanzania,Mikolag Kucia akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam namna malipo yanavyofanyika hasa pale mtu anapopokea bidhaa mara baada ya kuiagiza mtandaoni.

Na Abraham Ntambara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search