Kufungiwa Gazeti la Raia Mwema kwa Mwibua Lema na Utabiri Mzito...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
BAADA ya kufugiwa kwa Gazeti la Raia Mwema jana na Serikali kwa siku 90, Kumemuibua Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na kutabiri kuwa Kanuni za Maudhui ya Utangazaji zitakapoanza kutumika nchini hatutakuwa tofauti na nchi ya Korea Kaskazini.
"Raia Mwema limfugiwa kabla kabla #KanunuZa MaudhuiZaUtangazaji hazijaanza kutumika.Zikianza kutumika tofauti yetu na North Korea itakuwa haipo," amesema Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.
"Raia Mwema limfugiwa kabla kabla #KanunuZa MaudhuiZaUtangazaji hazijaanza kutumika.Zikianza kutumika tofauti yetu na North Korea itakuwa haipo," amesema Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Jana Serikali ililifungia Gazeti hilo kwa siku 90 kwa madai kuwa limeandika habari ya kumchafua Rais John Magufuli. Kufungia kwa Raia Mwema inaweka rekodi ya ndani ya siku 10 kufungiwa kwa magazeti mawili kwani tayari wiki iliyopita lilifungiwa gazeti la Mwanahalisi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo,Dk Hassan Abbasi kwa vyombo vya habari inasema serikali imefikia hatua kulifungia gazeti la Raia Mwema kutokana kuandiika nukuu ya uongo kwa Rais Magufuli.
Amesema toleo la namba 529 la terehe 27 semptemba hadi Oktoba mwaka ilichapisha habari ya Uchambuzi inayosema “URAIS UTAMSHINDI JOHN MAGUFULI”
Na Abrahama Ntambara
No comments:
Post a Comment