Mbunge Lazaro Nyalandu: Madaktari Nairobi Kalamu zao Nzito Kuandika Ripoti Mwenendo matibabu ya Lissu...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
MBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kwamba wamekuwa
wakisubiri Madaktari watoe ripoti ya mwenendo wa matibabu ya Tundu Lissu ili
kuwapatia Madaktari Bingwa wa Marekani.

Ameeleza hayo kupitia ukurasa wake
wa Facebook na kudai kuwa ripoti hiyo ni kwa ajili ya kuona uwezekano wa Lissu
kupatiwa rufaa kwa matibabu zaidi nje. Lakni amebainisha kuwa kalamu zao
zimekuwa nzito kuandika kuiandika kwa siku tatu tangu waahidiwe.
Kupitia Ukurasa wake wa Facebook ameandika “Tumekuwa #NairobiHospital tukisubiri
MADAKTARI watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa
minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh
#TunduLissu kupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni
nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe,”.
“Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya
uwezekano wa kumhamishia Mh TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora
zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospital wangeridhia. Kesho asubuhi
nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI
hiyo,” .
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment