Mbunge Msigwa Ashangaa Takukuru Kushindwa Kuwahoji Mbunge Msukuma na RPC Geta..Ni Kutokana na Kauli Tata ya Msukuma Dhidi ya RPC..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360
MBUNGE wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Peter Msigwa amezidi kushikilia suala la Mbuge wa Geita
Mjini na RPC wa Geita na kusema kuna jambo kati yao lakini anashindwa kuelewa
inakuaje mbaka sasa TAKUKURU inashindwa kuwahoji wote wawili.
Msigwa amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter zikiwa
zimepita siku kadhaa toka Mbunge na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph
Msukuma kudai kuwa ana siri nyingi za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli
Mwabulambo na kudai atazitoa siri hizo ikiwa Kamanda wa Polisi huyo hatamuomba
msamaha kwa kitendo alichomfanyia ikiwa pamoja na kumkamata na kumlaza rumande.
"Msukuma amesema anajua siri za RPC wa Geita , TAKUKURU
kwa nini hamjiongezi kuwahoji wote wawili, kuna kitu hakipo sawa kinaendelea
hapa" ameandika Msigwa.
Mbunge wa Geita alikamatwa na jeshi la polisi na kulazwa
rumande kwa masaa 24 kufuatia vurugu zilizofanywa katika mgodi wa Geita Gold
Mine (GGM) lakini alipotoka Mbunge huyo alianza kumshtumu RPC wa Geita na
kusema anafahamu mambo yake mengi, akahitaji kuombwa msamaha ndani ya siku tatu
na RPC huyo huku akiahidi kutoa siri zake kama hatafanya hivyo.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment